Afisa wa zamani wa jeshi la Muungano wa Usovieti aliyefanikiwa kutoa ushawishi mkubwa wa kutofanyika kwa vita vya nyuklia kati ya Marekani na Muungano huo wakati wa Vita Baridi amefariki dunia akiwa na miaka 77.

Stanislav Petrov ambaye alikuwa zamu katika kituo cha Urusi cha kujihami na makombola ya nyuklia, mapema siku moja mwaka 1983 mitambo ya kompyuta ilifanya makosa na kutoa taarifa kuwa kuna makombora yaliyokuwa yamerushwa na Marekani kuelekea Urusi.

Aidha, Petrovic alichukua uamuzi wa kuutangazia umma kuwa taarifa hiyo haikuwa sahihi na kutoa ripoti kwa wakuu wa jeshi ambao tayari walikUwa tayari wameshaanza maandalizi ya kujibu mapigo,

“Nilikuwa na nyaraka zote, kudokeza kwamba kulikuwa na shambulio la makombora ambalo lilikuwa linaendelea, iwapo ningeituma ripoti hiyo kwa wakubwa wangu, hakuna yeyote ambaye angezitilia shaka,” amesema Petrov

Hata hivyo, baada ya kufanyika kwa uchunguzi kuilibainika kuwa satelite za Umoja hu wa Usovieti zilikuwa na hitilafu iliyosababisha kutoa taarifa ambazo hazikuwa sahihi kuhusu makombora ya nyuklia.

Mbunge Musukuma na wenzake wapandishwa kizimbani
Mlinda amani raia wa Tanzania auawa nchini Congo