Imefahamika kuwa kesi iliyopelekea uchaguzi mkuu wa TFF usimamishwe na Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam, imefunguliwa na aliyekuwa mgombea Urais wa TFF kutoka Tanzania visiwani (Zanzibar) ndugu Ally Saleh.
Leo Alhamis jioni Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam ilipokea kesi ya kupinga uchaguzi wa Shirikisho wa Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Pia imemtaka Rais wake Wallace Karia, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi na Bodi ya Wadhamini ya Shirikisho hilo kufika Mahakamani hapo kujibu hoja za kwa nini uchaguzi wa TFF usisimamishwe.
Wahusika wametakiwa kuitikia wito huo kabla ya kesho Ijumaa saa 3 asubuhi.
Ally Saleh aliyenguliwa kwenye kinyang’anyiro cha Urais wa TFF kwa kutokukidhi kanuni ya kuwa na wadhamini watano, amewahi kushika nyazifa mbalimbali ikiwemo ubunge pia amewahi kuwa mwandishi wa habari wa (BBC).