Baba mmoja nchini India amemkata na kuondoa kabisa mikono yote miwili  kijana mmoja mwenye umri wa miaka 17 anayetuhumiwa kumbaka mtoto wake wa kike mwenye umri wa miezi 7 tu.

Kwa mujibu wa Daily Mail, baba huyo anadaiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa anajiandaa kuelekea mahakamani kusikiliza kesi yake. Imeelezwa kuwa alimfunga kamba kwenye mti kijana huyo kabla ya kumkata mikono yote na kumtelekeza karibu na mfereji.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa mwaka 2014, mama wa mtoto huyo alimshuhudia kijana huyo akimbaka mtoto huyo.

Majeruhi 2

Jeshi la Polisi limemtaja baba huyo kama Parminder Singh, na kwamba ametekeleza tukio hilo April 19 mwaka huu wakati ambapo mtuhumiwa alipaswa kufika mahakamani kwa ajili ya kusikiliza kesi yake.

Jeshi hilo limesema kuwa limeanza msako mkali kuhakikisha wanamtia mbaroni baba huyo na kwamba mhanga wa tukio hilo anaendelea na matibabu na afya yake inaimarika.

Polisi wanamsaka baba huyo mwenye umri wa miaka 25 waiwa na dhamira ya kumpandisha mahakamani kwa kosa la jaribio la mauaji.

 

WAZIRI MKUU AONGOZA WAKAZI WA DODOMA MAZISHI YA ASKOFU ISUJA
Jerry Muro: Leo Tutalipiza kisasi cha Kipigo cha Azam FC Tunisia