Kampeni za uchaguzi mkuu zinaendelea ambapo leo mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli alikuwa Babati, Manyara akinadi ilani ya chama hicho na kuwasihi wananchi kumchagua yeye wapate maendeleo ya kweli.

Pamoja na kupokea changamoto mbalimbali kutoka kwa wananchi wa Babati, Masikio ya Dk. Magufuli yalikutana na malalamiko ya mgombea ubunge wa Babati Mjini, Mh. Chambili ambaye alimueleza kuhusu sakata la mbunge wa viti maalum wa Chadema kuwafikisha polisi viongozi wa CCM kwa madai kuwa walitaka kumbaka.

Ingawa hakumtaja jina, Mh. Chambili alieleza kuwa mbunge huyo alieleza kuwa alitaka kubakwa na viongozi wawili wa CCM ndani ya Mkutano wa Halmashauri, hivyo, alipendekeza kuwa ni vyema watu wawe wanapimwa akili kabla ya kupewa uongozi.

Aidha, Chambili alimuomba Dk. Magufuli, endapo ataingia madarakani asaidie kulifikisha fungu kwa ajili ya maendeleo ya jimbo la Babati ambayo yako kwenye mipango kwa muda mrefu.

Awali, Dk. Magufuli aliwaahidi wananchi wa Babati kuwa wamchague yeye kwa kuwa amepanga kuleta maendeleo ya kweli kwao na kuahidi kuinua uchumi wa kila mmoja kupitia uimarishaji wa miundombinu pamoja na viwanda atakavyojenga na kufufua nchi nzima.

Dk. Magufuli aliutaka umati uliohudhuria katika mkutano huo kuwapuuza wagombea wa vyama vingine kwa kuwa ahadi zao hazitekelezeki na kwamba wamejaa lugha za matusi.

Tanzia: Kama Sio Ajali Ya Gari, Ndoto Hizi Za Mtikila Huenda Zingetimia
Chadema wamgomea tena Jaji Lubuva, Macho Yote Kituo Cha Kura