Dennis Itumbi ameachiliwa huru baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma – DPP, Noordin Haji kuondoa kesi hiyo Mahakamani kutokana na kukosekana kwa ushahidi dhidi ya madai ya kula njama ya kumuua Rais William Ruto mwaka 2021 alipokuwa Naibu Rais.
Hakimu wa Mahakama jijini Nairobi nchini Kenya, amesema upande wa mashtaka ulikuwa na utaratibu mbaya na haramu kwenye mchakato mzima wa kesi hiyo.
Kesi ilikuwa imewasilishwa mahakamani kwamba Bw Itumbi alisambaza barua feki ikiibua madai ya kuwepo kwa njama ya kumuangamiza Dkt Ruto.
Utawala wa Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta, ndio uliolaumiwa zaidi kwa sababu baadhi ya mawaziri kwenye serikali hiyo, walitajwa kupanga njama hiyo.