Kiungo kutoka nchini Hispania na klabu ya Man Utd, Ander Herrera amewapiga kijembe mahasimu wao wa mjini Manchester, Man City kwa kusema kikosi cha mashetani wekundu ni bora kuliko cha matajiri hao.

Herrera ametupa dongo hilo, kufuatia kitendawili kilichopo hivi sasa cha kuwania nafasi nne za juu katika msimamo wa ligi kuu ya soka nchini England, ambapo Man Utd wameonyesha wanaweza kupambana na kuiondoa Man City katika mpango huo.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26, amesema hana shaka na kikosi chao katika suala la kumaliza katika nafasi nne za juu, kutokana na kasi waliyonayo hivi sasa ambayo imekua tishio, tofauti na ilivyokua siku kadhaa iliyopita.

Man Utd ipo katika hati hati hiyo, baada ya kukosa kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu wa 2014-15, kutokana na matokeo mabaya yaliyowaandama chini ya David Moyes, na hiyo ilikua ni mara ya kwanza kushindwa kutinga kwenye michuano hiyo tangu mwaka 1995.

“Man United ni lazima icheze michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kila mwaka na kilichotokea miaka miwili iliyopita kwa kukosa michuano hiyo ilikua ni kama bahati mbaya kwetu,” Alisema Herrera.

“Sisi ni Man United, na kila mchezaji anatambua anachotakiwa kufanya, hivyo ninakuhakikishia Man city hawatoweza kushindana nasi katika mbio za kumaliza nne bora.” Aliongeza Herrera

Man utd wamesaliwa na ratiba ya michezo kadhaa, ambapo miongoni mwa michezo hiyo watapambana na wanaowania ubingwa Tottenham, katika uwanja wa White Hart Lane.

Gardner G Habash arejea Clouds Fm
Inter Milan yajizatiti Kwa Yaya Toure