‘Kuachwa ni shughuli pevu na ukiona mwanaume analia ujue kuna jambo’, hiki ndicho kinachomkuta mwigizaji maarufu, Brad Pitt ambaye baada ya kumwagwa na Angelina Jolie amekuwa akilia machozi kama mtoto awapo mbali na macho ya umma, kwa mujibu wa  chanzo cha Weekly Source.

Taarifa zimeeleza kuwa Angelina Jolie ambaye Septemba 19 aliwasilisha maombi ya talaka mahakamani amempa adhabu nyingine kubwa Pitt baada ya kumfungia mawasiliano yote ya simu na mitandao.

“Angelina ameblock namba zote za simu za Pitt,” chanzo hicho cha karibu kinakaririwa na Weekly Source. “Brad Pitt ameshindwa kuvumilia, amekuwa akilia mwenyewe. Hakuwa anafikiria kama Angelina angefanya haya,” kiliongeza.

Kuongeza uzito wa adhabu, imeelezwa kuwa Angelina Jolie amekodi jumba la kifahari Malibu ambapo amewatunza humo watoto wake wote kwa makubaliano ya kutotoka nje akiwaweka mbali na Brad Pitt.

Angelina Jolie aliamua kumpiga chini Brad Pitt akidai alichepuka na mrembo Marion Cotillard. Ingawa mrembo huyo aliweka wazi kupitia mitandao ya kijamii kuwa mimba aliyonayo sio ya Brad Pitt, bado ushawishi wote haulikuni sikio la Angelina Jolie.

Marion aliyevunja ndoa ya Brad Pitt

Marion aliyevunja ndoa ya Brad Pitt

Slaven Bilic: Haya Ni Mapito, Tutarudi Njia Kuu
Nyumba za starehe, nyumba za ibada na baa marufuku mikesha, mwisho saa tano