Pambano la uzito wa juu baina ya Anthony Joshua na Carlos Takam lililopigwa usiku wa kuamkia leo mjini Cardiff limemalizika kwa Joshua kutetea ubingwa wake wa WBA ‘super’ na IBF baada ya kumpiga Carlos Takam kwa TKO ‘Technical knock out’ raundi ya 10.
Joshua mwenye umri wa miaka 28 aliumia pua raundi ya pili baada yakugongana kichwani na mpinzani wake lakini hatua kwa hatua alizidi kuimarika na kufanikiwa kumchapa Carlos Takam raundi ya 10.
Huu ni ushindi wa 20 mfurulizo kwa Anthony Joshua kushinda kwa ‘knock out’ baada ya kumtwanga Wladmir Klitschko mnamo mwezi Aprili katika uwanja wa Wembley.
-
Anthony Joshua Ampa Kichapo Klitschko
-
Yanga, Simba zatoka suluhu huku Kichuya akiweka rekodi ya aina yake
-
Moto wa Man City hauzimiki, Liverpool, Arsenal nao kifua mbele
Raundi ya 10 Joshua alionekana kumshambulia Takam kwa nguvu huku makonde mengi yakimpata Takam moja kwa moja na mwamuzi wa pambano hilo kuamua kumaliza pambano jambo ambalo liliwashangaza wengi wakidai mwamuzi alimaliza pambano mapema baada ya kuona Takam akizidiwa.