Mwanaume mmoja nchini Saudi Arabia amenyongwa kwa uhalifu ambao kwa mujibu wa makundi ya kutetea haki za binadamu, aliyafanya akiwa na umri wa miaka 17.
Mustafa Hashem al-Darwish alikamatwa mnamo mwaka 2015 kwa makosa yanayohusiana na maandamano.
Mamlaka nchini Saudia zinasema alishtakiwa kwa kuunda seli ya kigaidi na kujaribu kufanya uasi kwa kutumia silaha.
Licha ya makundi ya kutetea haki kutoa wito wa kutotekelezwa kwa adhabu ya kifo dhidi yake, yakisema kesi yake haikuwa ya haki, ufalme wa nchi hiyo pia umekuwa ukijinasibu kwamba umekomesha adhabu ya kifo kwa watoto.
Mashirika ya kutetea haki ya Amnesty International na Reprieve, ambayo yanapinga adhabu ya kifo, yanasema al -Darwish ambaye alikuwa na umri wa miaka 26, alikiri makosa hayo baada ya kudai wa kuteswa. Mamlaka ya Saudi Arabia haijatoa tamko lolote hadharani juu ya tuhuma hizo.
Kulingana na shiririka la habari la Reuters, mashataka dhidi ya al-Darwish yalijumuisha “kutaka kuvuruga usalama kupitia maandamano” na “kuzua ugomvi”.
Ushahidi dhidi yake ulijumuisha picha “ya kukera kwa vikosi vya usalama”, na ushiriki wake katika mikusanyiko zaidi ya 10 ya “ghasia” mnamo mwaka 2011 na 2012.