Mwenge wa Uhuru  umeanza kukimbizwa katika Mkoa wa Arusha ambapo utakapokuwepo Mkoani humo, utaweka mawe ya msingi,kuzindua, kufungua na kukagua miradi 53 ya maendeleo  yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 581.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amepokea Mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere katika kijiji cha Kansay kilichopo Wilaya ya Karatu.

Mwenge wa Uhuru  unatarajiwa kupita katika miradi nane yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilion 3.4, katika wilaya ya Karatu.

Miongoni mwa miradi hiyo ni wa Ujenzi wa maabara ya kisasa katika kituo cha afya cha Endabash, pamoja na mradi wa matumizi sahihi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(Tehama) .

Mwenge unatarajiwa kukimbizwa kwa jumla ya kilometa950.35 katika mkoa wa Arusha kwa siku sita katika wilaya sita.

Fid Q amfungukia Nandy na tamasha lake
Masau Bwire aitumia salaam Young Africans