Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Masuala ya Utalii [UNWTO], limeikubali Tanzania kuwa mwenyeji mkutano ujao wa maswala ya utalii Bara la aAfrika ambapo pia wameingiza Tanzania kuwa nchi ya tatu itakayowezeshwa mradi mkubwa wa Utalii

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damasi Ndumbaro ambapo amebainisha kuwa, Ujumbe wa Tanzania umeweza kupata faida hizo mbalimbali  sambamba na kupata uzoefu mkubwa ikiwemo pia kutangaza fursa za Utalii za Tanzania katika mkutano huo ambao una wadau wakubwa wa Utalii.

“Tumekutana nchi nyingi za Kiafrika, tumejadili mambo mengi, tumebadilishana uzoefu mkubwa tumepata mawasilisho mbalimbali kutoka kwenye makampuni yenye uwezo wa juu kabisa wa kutangaza utalii duniani.

”Pia tumepata fursa ya kufanya mikutano ya ana kwa ana na wadau mbalimbali moja kati ya wadau hao ni Katibu Mkuu ambaye anayeshughulikia masuala yaUtalii wa Umoja wa Mataifa Bw. Pololikashvili, ambaye amekubali mkutano ujao wa Utalii Barani Afrika, ufanyikie Tanzania”. Alisema Dkt. Ndumbaro.

Ndumbaro, amesema wameweza kuomba na kukubaliwa kuiingiza Tanzania kuwa  moja kati ya nchi tatu Barani Afrika ambazo zitapata mradi wa Umoja wa Mataifa kwenye masuala ya Utalii.

“Nchi zingine zikiwa Namibia na Cape Vede ambazo zimeshaingizwa toka zamani kwa namna ya kipekee Tanzania tumepewa upendeleo huo baada ya kushiriki hapa na tayari tutaingizwa katika mradi huo mkubwa”. amesema Ndumbaro.

Shoti ya umeme yakatisha maisha ya wanandoa waliotoka fungate
Ajibu aachwa Dar es salaam