Kiungo mshamhuliaji wa Simba SC, Ibrahim Ajibu ameachwa jijini Dar es salaam, wakati kikosi cha mabingwa wa Tanzania Bara kikielekea jijini Mwanza, kwa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Polisi Tanzania FC.

Simba SC watakua wageni wa Polisi Tanzania FC mwishoni mwa juma hili, katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Ajibu hakuwa sehemu ya kikosi cha Simba SC kilichoondoka mchana wa jana Jumatano jijini Dar es salaam, na kuwasili Mwanza saa tisa alasiri.

Katika mazoezi ya kikosi cha Simba ya mwanzoni mwa juma hili kabla ya kuelekea Mwanza, kocha Didier Gomes alisema Ajib ni mgonjwa.

Simba SC imekwenda Mwanza huku ikiwa kileleni mwa msimamo mwa Logi Kuu Tanzania Bara, kwa kumiliki alama 67 zilizopatikana kwenye michezo 27 iliyocheza hadi sasa.

Tanzania mwenyeji mkutano ujao utalii Afrika
RC Shigella awapiga marufuku mgambo kuwabughudhi wafanyabishara