Wanandoa wapya Zaheer Sarang na Nabeelah Khan (24) wamefariki dunia kwa shoti ya umeme huko Afrika kusini ikiwa ni siku moja tu tangu watoke kula fungate ‘honeymoon’.

Kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa katika mtandao wa Sunday world, Msemaji wa polisi wa jimbo la Guetang, Mavela Masondo ameeleza kuwa miili ya wanandoa hao iligunduliwa bafuni kwao Jumapili Juni 13, mwaka huu.

Imeelezwa kuwa wanandoa hao wakiwa bafuni mke huyo alishika tap (switch), akapigwa na shoti ya umeme ambapo mume alipojitosa kumuokoa na yeye akaunganishwa katika shoti hiyo wakafariki wote.

Inaaminika watu katika eneo hilo hupenda kujiunganishia umeme kiholela kinyume cha sheria na hivyo kusababisha majanga kama hayo.

Mkurugenzi wa nishati wa mji wa mji huo, Mongezi Ntsokolo ameagiza kufanyika kwa uchunguzi wa haraka katika eneo hilo.

Polisi wamesema bado wanaendelea kuchunguza zaidi tukio hilo kwa kushirikiana na mamlaka inayohusika kusambaza umeme katika jimbo la Guetang.

Masau Bwire aitumia salaam Young Africans
Tanzania mwenyeji mkutano ujao utalii Afrika