Mwanamuziki maarufu wa HipHop Farid Kubanda maarufu Fid Q amesema kuwa wasanii wa kike katika muziki wa bongo ni wachache hivyo wanapotokea kuonesha juhudi za kukuza muziki wa bongo wapate sapoti, kama ambavyo nchi zingine wanafanya.

Fid Q amesema kuwa muziki wa bongo wananume ndiyo wanatawala na kunaidadi ndogo ya wanamuziki wa kike, ambapo ameshauri wanapotokea wenye juhudi za kusapoti muziki wa bongo kama Nandy waungwe mkono.

“Wasanii wa kike Tanzania wachache sana lazima wapewa sapoti natarajiwa iwe kubwa zaidi miaka ijayo na naamini watu Wataipokea vizuri, tunahitaji kuwa na wasanii wakubwa wa kike ili sanaa iwe stable, na ndio maana nimekuja kumpa sapoti Nandy kwenye jambo lake”amesema Fid Q

”Nady Festival natamani iwe kubwa zaidi ya mwaka nhuu miaka ijayo” amesema Fid Q

Anyongwa mpaka kufa kwa uhalifu alioufanya utotoni
Mwenge wa Uhuru kukagua miradi yenye thamani ya bilioni 581