Mwanamuziki maarufu nchini Marekani Faheem Rasheed Najm maarufu T-Pain amefunguka namna alivyokataliwa kufanya kolabo ya wimbo na mkali wa Hip Hop Onika Tanya Maraj maarufu Nicki Minaj mwaka 2007.

Katika kipindi cha Mahojiano cha Desus & Mero, T-Pain amesema kuwa mwaka huo ndiyo kipidi Nicki Minaj anaanza muziki ambapo alikuwa akimtafuta msanii huyo bila mafanikio.

T- Pain amesema kuwa alivunjika moyo kwa kitendo cha Nicki Minaj kuanza kumchunia mkali huyo na kwa kutojibu meseji zake.

“Alikuwa akinijibu, ‘Unajua mimi ni msanii pia na ninafanya kazi zangu, kwa hiyo unajua hebu tulia kwanza.’ ” ameeleza T-Pain akimnukuu Nicki Minaj.

T- Pain amesema kuwa alimuomba verse walau moja tu kwenye nyimbo yake Nicki Minaj aliendelea kujibu vile vile: “I’m working on my sh!t too.”

Nicki Minaji kupitia ukurasa wake wa Twetter ameandika kuwa hakumbuki kufanya kitendo hicho lakini kama ni kweli basi anajishangaa kwanini alikataa Kolabo na msanii mkubwa kama T-Pain tena kipindi ambacho alikuwa bado hajatoka kimuziki.

Simba SC washindwa kuvumilia, watinga Chamazi
Kaizer Chiefs kuhusu Kambole kutua Young Africans