TAARIFA za chini ya kapeti zinaeleza kuwa, Uongozi wa Klabu ya Simba umeufuata uongozi wa kikosi cha klabu ya Azam kwa ajili ya kuomba kuachiwa nafasi ya kumsajili aliyekuwa beki wa Ruvu Shooting, Edward Charles Manyama.

Azam FC tayari wamemtangaza Manyama kuwa mchezaji wao mpya kwa mkataba wa miaka mitatu, huku wakati huohuo Simba walikuwa wakitajwa kumalizana na nyota huyo.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya kikosi cha Azam FC kimelitonya Championi Jumatatu, kuwa Simba wameufuata uongozi wa Azam kuomba kuachiwa mchezaji huyo.

“Unajua ishu ya Manyama kuhitajika na Simba ni jambo lililo na uzito mkubwa sana kiasi kwamba, kuna baadhi ya viongozi wao wamekuja kujaribu kuongea na viongozi wetu ili tuwaachie, lakini tayari uongozi wetu uliwaambia tuna mipango naye.

Alipotafutwa Ofisa habari wa Klabu ya Azam, Zakaria Thabit, Zaka Zakazi kuzungumzia suala hilo alisema:  “Watu wengi hawajui kuwa sisi Manyama tulimalizana naye mapema, kabla ya hizo tetesi za klabu ya Simba kumhitaji, hivyo ninachojua mimi Manyama ni mchezaji wetu na si vinginevyo.”

Usajili wa Manyama umekuwa na mvutano mkubwa ambapo habari za awali zilieleza kuwa Simba imemalizana na nyota huyo kwa dili la miaka miwili ilibaki suala la kumtangaza.

Kabla dili lake halijatangazwa, Azam FC walifanya yao kwa kumtambulisha rasmi nyota huyo kwa kueleza kuwa wamempa dili la miaka mitatu.

Manyama aliibukia ndani ya Ruvu Shooting akitokea Klabu ya Namungo FC iayonolewa na Kocha Mkuu, Hemed Seleman.

Chanzo: Saleh Jembe

Simba SC kuifuata Polisi Tanzania
T- Pain: Nicki Minaji alinikatalia kolabo kipindi anaanza muziki