Klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini imeshatushwa na taarifa zinazomuhusu Mshambuliaji wao kutoka nchini Zambia Lazarous Kambole, anayetajwa kukaribia kutua Young Africans ya Tanzania.

Kwa siku kadhaa baadhi ya vyombo vya habari vya Tanzania vimekua vikimuhusisha Mshambuliaji huyo aliekosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Kaizer Chiefs, kujiunga na Young Africans kwa mkopo wa mwaka mmoja, huku ikisemekana viongozi wa klabu hizo wameshaanza mazungumzo.

Afisa habari wa Kaizer Chief Vinna Maphossa amesema kuwa taarifa zinazosemwa kuwa Mchezaji wao Lazarous Kambole anahitajika Young Africans, sio za kweli na kama itatokea Uongozi wa klabu hiyo ya Tanzania utahitaji mazungumzo ya kumsajili Kambole, watathibitisha kupitia kwenye vyanzo vyao vya habari.

“Bado hatujapata taarifa rasmi kuhusiana na suala hilo,litakapotufikia tutaweka wazi, bado tuna mkataba na Kambole na kwasasa Tunatazama michuano mikubwa ya nusu fainali iliyoko mbele yetu kwahiyo hiyo taarifa bado haijatufikia kwa sasa.” amesema Vinna Maphosa.

Kaizer Chiefs ilimsajili Kambole mwaka 2019 akitokea ZESCO United ya nchini kwao Zambia, baada ya kuonesha uwezo mkubwa kisoka, lakini tangu alipotua Amakhosi, amekua na wakati mgumu wa kulishawishi benchi la ufundi ili kuingia kwenye kikosi cha kwanza.  Ameshacheza michezo 14 akiwa na Kaizer Chiefs, na amefunga bao moja mpaka sasa.

T- Pain: Nicki Minaji alinikatalia kolabo kipindi anaanza muziki
Watatu wahukumiwa kunyongwa hadi kufa Kigoma