Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma imewatia hatiani washtakiwa watatu ambao ni Nuru Venevas, Seth Simon na Ezekiel Kalobezi na kuwahukumu kunyongwa hadi kufa kwa kosa la mauaji.

Mshtakiwa Nuru Venevas na wenzake wawili walifanya tukio hilo mnamo tarehe 2 Oktoba, 2016 majira ya usiku katika Kijiji cha Kwaga, Wilaya ya Kasulu iliyopo Mkoani Kigoma ambapo walimvamia marehemu na walinzi wenzake wakiwa wanalinda mitambo ya kutengeneza barabara ya Kasulu-Kigoma.

Washtakiwa hao walimuua marehemu kwa kumkatakata na panga kisha kuiba control box ya excavator (sanduku la mchimbaji wa barabara) ambayo mshtakiwa Seth Simon alikamatwa nayo Mkoani Geita.

Hukumu hiyo ya iliyotolewa mbele ya Jaji Matuma katika kesi ya mauaji Namba 36 ya mwaka 2020 imetolewa mahakamani hapo baada ya ushahidi uliotolewa na Jamhuri.

Kesi hiyo iliendeshwa na Mawakili wa Serikali Robert Magige na Edna Makala, ambapo upande wa utetezi uliongozwa na Sadick Aliki akiwa pamoja na Dennis Kayaga.

Kaizer Chiefs kuhusu Kambole kutua Young Africans
Banda: Mkude, ana uwezo wa kucheza Afrika Kusini