Nguli wa muziki wa RnB Duniani, R Kelly amewatimua kazi mawakili wake wawili, Steve Greenberg na Michael Leonard ikiwa ni miezi miwili kabla ya kesi yake kusikilizwa.

Kupitia kikao kifupi na Mahakama mapema wiki hii, R Kelly ameeleza kuwa amewafuta kazi mawakili hao kwa sababu hawakuwa vizuri kwenye suala la uwajibikaji na amepanga kuongeza timu ya wanasheria wapya ili kuziba nafasi hizo zilizoachwa wazi mapema kabla ya kesi yake.

R Kelly amemthibitishia Jaji wa Mahakama, Ann Donnelly kwamba ataendelea kufanya kazi na timu ya wanasheria wake Becker na Farinella ambao wamesalia kwenye ile timu ya watu wanne ili kushughulikia kesi yake inayomkabili ya unyanyasaji wa kingono.

Kelly, ambaye alikuwa miongoni mwa nyota maarufu wa muziki aina ya RnB miaka ya 1990, amekuwa gerezani kwa takriban miaka miwili wakati akisubiri kusikilizwa kwa kesi yake huku kesi zilizowasilishwa dhidi yake zikiwa Illinois, Minnesota na New York.

Amenyimwa dhamana mara tatu na hakimu wa Brooklyn alisema kuna uwezekano mkubwa ushahidi kuingiliwa katika kesi ambapo anadaiwa kuongoza kundi la uhalifu kwa muda mrefu kusajili wanawake na wasichana kufanya na mapenzi nao.

Mtanzania aliyepanda Mlima Everest arejea nchini, aeleza siri ya mafanikio yake
Boss wa IPTL kupelekwa mahakama ya Hakimu Mkazi