Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson amefunga ndoa na Carrie Symonds katika sherehe ndogo iliyofanywa kwa siri huko Westminster Cathedral.

Boris anakuwa Waziri Mkuu wa kwanza kufunga ndoa akiwa anaitumikia ofisi ikiwa imepita takribani miaka 200 tangu kutokea kwa tukio la aina hiyo.

Wawili hao walifunga ndoa jana Jumamosi Mei 29, 2021 huku Waziri wa Biashara na Viwanda na Upelekaji wa Chanjo ya COVID, Nadhim Zahawi akisema hakuhudhuria sherehe hiyo lakini amewatakia kheri katika ndoa yao.

“Ninadhani ni jambo la kufurahisha kwa wote wawili kuweka nadhiri zao za ndoa, ninawatakia kila la kheri,” amesema Zahawi.

Ingawa Boris alishawahi kufunga ndoa mara mbili, Kanisa Katoliki linaruhusu watalaka kufunga ndoa nyingine iwapo viapo vya ndoa za zamani vililiwa nje ya kanisa hilo.

Hussein Machozi ajibu madai ya kuolewa Italia
Vikwazo 34 biashara 'out'