Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Low ameomba radhi baada ya kuonekana katika video na picha mbalimbali zilizosambaa akiingiza mkono sehemu zake za siri na kisha kunusa.
Katika mchezo dhidi ya Ukraine ambao ulishuhudia Ujerumani wakishinda mabao 2-0, Low alionekana akiingiza mkono sehemu zake za siri (nyuma na mbele ) na kuuweka puani pamoja na mdomoni.
Lukas Podolski amemtetea kocha wake, huku Low mwenye akisema kuwa hakuwa anajitambua wakati akifanya hivyo.
“Ni kweli nimeona hizo picha na kimsingi sikua najitambua lakini hata hivyo nitajaribu kuhakikisha sirudii tena kufanya hivyo. Nisameheni sana kwa hilo,” amesema Low.
Picha zikimuonyesha Joachim Low akiingiza mkono sehemu zake za siri na kisha kunusa, wakati wa mchezo wa Euro 2016 dhidi ya Ukraine.

 

Video: Rais Magufuli amewatakia Waislamu wote Mfungo mwema wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani
Picha: Roberto Di Matteo Atambulishwa Rasmi