Washika bunduki wa kaskazini mwa jijini London, Arsenal wameondoka katika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka nchini England, na kuweka makazi katika nafasi ya sita kufuatia ushindi wa bao moja kwa sifuri walioupata dhidi ya mabingwa watetezi Leceister City usiku wa kuamkia leo.

Bao pekee lililoamua matokeo ya mchezo huo lilipatikana dakika ya 86 ya mchezo, baada ya mlinzi wa Leceister City, Robert Huth kujifunga akiwa katika harakati za kuokoa shuti la mlinzi wa kushoto wa Arsenal, Nacho Monreal.

Ushindi huo umeifanya Arsenal ifikishe pointi 60 baada ya kucheza michezo 32,  ikiwa ni pointi mbili mbele ya Everton iliyoshuka mpaka nafasi ya saba. Everton imecheza michezo 33.

Katika mchezo mwingine, Tottenham waliibuka na ushindi wa bao 1-0 ugenini kwa kuwafunga wenyeji wao Crystal Palace. Shukrani kwa bao la kiungo Christian Erikssen.

Middlesbrough wakiwa nyumbani Riverside waliifunga Sunderland bao 1-0 katika dakika ya 8.

Paris St-Germain Waisasambua AS Monaco
Live: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Aprili 27, 2017