Mabingwa wa soka Ufaransa, Paris St-Germain wamewabomoa vinara wa ligi ya soka nchini humo AS Monaco kwa kwa mabao matano kwa sifuri, katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la ligi uliochezwa usiku wa kuamkia leo, kwenye dimba la Parc des Princes jijini Paris.

Mabao yaliyowapa ushindi Paris St-Germain, yalifungwa na Julian Draxler, Edinson Cavani, Blaise Matuidi, Safwan Mbae aliyejifunga na Marquinhos.

Ushindi huo umeipeleka Paris St-Germain hatua ya fainali kwa mara ya tatu mfululizo na watacheza na Angers, huko Stade de France Mei 27 mwaka huu.

Angers wamefuzu hatua ya fainali kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 60 baada ya Jumanne usiku kuifunga Guingamp mabao 2-0.

FC Bayern Munich Watupwa Nje DFB Pokal
Arsenal Wahama Mtaa Wa Saba