Gwiji wa klabu ya Arsenal Thierry Henry, ametangaza kuachana na The Gunners baada ya kutoafitiana na bosi wake Arsene Wenger, kufuatia kushindwa kufanya maamuzi ya kuendelea kuwa kocha wa vijana wa klabu hiyo ama kubaki kuwa mchambuzi wa kituo cha runinga cha Sky Sports

Kituo cha televisheni cha Sky Sports kinamlipa Henry kiasi cha paundi milioni 4 kwa mwaka kama mshahara.

Taarifa za ndani zinadai kwamba kitendo cha Henry kuikosoa Arsenal, mara kwa mara hasa safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Olivier Giroud, kimekua sababu ya Wenger kumtaka aondoke.

Henry amewahi kusema kwamba Arsenal wasingeweza kubeba ubingwa wa ligi ya nchini England, endapo wangeendelea kumtegemea mshambuliaji Giroud.

Wenger, ambaye hutumiwa mara kwa mara na kituo cha Televisheni cha TV beIN Sports kama mchambuzi aliifikisha Arsenal nafasi ya pili nyuma Leicester kwa tofauti ya point kumi.

Hata hivyo maamuzi ya Arsene Wenger ya kumtimua Henry, yamewashangaza wadau wengi wa soka hasa ukizingatia historia kubwa aliyonayo gwiji huyo klabuni hapo.

Imefikia hatua mpaka baadhi ya watu kusema kwamba inawezekana Wenger ana hofu ya kunyang’anywa tonge mdomoni kutokana na mkataba wake kusalia mwaka mmoja.

Henry aliahidiwa kupewa pesa katika kazi yake hiyo ya kukinoa kikosi cha vijana wenye umri chini ya miaka 18, licha ya kwamba alitaka kufanya kazi hiyo bure kabisa.

Akiwa na Arsenal, Henry alifanikiwa kubeba mataji mawili ya ligi ya England na Matatu ya FA, kwa kipindi cha miaka minane alichodumu klabuni hapo.

Alifunga mabao 228 kwenye michezo 376, hatua mbayo ilipelekea apewe heshima ya kujengewa sanamu nje ya uwanja wa Emirates.

Hivi karibuni mchezaji mwenza wa zamani Tony Adams alijiunga naye kama kocha msaidizi wa Henry katika kikosi hiko cha vijana.

Naibu Waziri Mpina Atoa Mwezi Mmoja kwa kiwanda Cha Twiga Cement Kurekesha Miundo Mbinu
Besigye akubaliwa Dhamana