Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amerejesha kijembe kwa wanaomdhiki, kwa kusema hafikirii kuachana na klabu hiyo kwa sasa na badala yake anajihisi ni mwenye hamasa kuliko miaka kadhaa iliyopita.

Wenger, amerejesha kijembe hicho, kufuatia baadhi ya mashabiki kuonyesha wamechoshwa na huduma yake ambayo imeshindwa kueleta tija kwenye klabu yao kwa msimu huu, ambapo walikua na matumaini makubwa ya kutetea taji la kombe la FA pamoja na kutwaa ubingwa wa nchini England.

Mzee huyo wa kifaransa amelazimika kulizungumza jambo hilo, baada ya kuulizwa swali na mwandishi wa habari wakati wa mkutano ambao ulikua na lengo la kuzungumzia mchezo wa hii leo dhidi ya FC Barcelona.

Amesema anafahamu hawezi kupendwa na watu wote, lakini anachojua wanaomkubalia ni wengi na wakati mwingine wanaompinga wamekua na homa za vipindi, kwa kuafiki anachokifanya na kumpinga kwa wakati fulani.

“Ninajua siwezi kupendwa na kila mmoja, lakini nafahamui vizuri kila mwenye mapenzi na klabu ya Arsenal kuna wakati tunakua pamoja na tunapongezana, lakini inapotokea tukiteleza kidogo, basi unaona baadhi yao wanajitenga na kunipinga” Alisema Wenger

Wenger, ameongeza kwamba anafahamu anachokifanya, na wakati mwingine anaamini hukosea kama binaadamu, lakini yote hayo ni masuala ya kawaida ambayo humtokea kila mja ambaye yupo duniani kwa maslahi ya walio wengi.

Thomas Mashali Autamani Ubingwa Wa Francis Cheka
Togo Wakubali Kucheza Mjini Monastir Kwa Idhini Ya CAF