Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amepanga kuwafukuzia viungo N’Golo Kante wa Leicester City pamoja na Granit Xhaka wa Borussia Monchengladbach wakati wa majira kiangazi.

Wenger amepanga mikakati hiyo, huku Ngolo Kante akimpa kipaumbele katika orodha ya wachezaji atakaowasajili siku za awali mara tu dirisha la usajili litakapofunguliwa mwishoni mwa msimu huu.

Uwezo na kujituma kwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25, ndio kilichomvutia babu huyo kutoka nchini Ufaransa ambaye ameshindwa kuiwezesha Arsenal kutwaa taji la nchini England kwa zaidi ya miaka kumi.

Wenger amemtanguliza Kante kwa kuamini itakua rahisi kumtumika katika ligi ya nchini England, kutokana na uzoefu alioupata msimu huu akiwa na  Leicester City wanaokaribia kutwaa taji la England.

Hata hivyo ameweka mkakati namba mbili wa kumnasa kiungo Granit Xhaka wa klabu ya Monchengladbach ya nchini Ujerumani, endapo atashindwa kufikia lengo la kumsajili Kante.

Granit Xhaka

Thamani ya Xhaka mwenye umri wa miaka 23, tayari imeshaanikwa wazi kuwa ni Pauni million 27.5, tofauti na ya Ngolo Kante ambayo inakadiriwa kufikia Pauni million 25.

Lengo kubwa la mzee huyo kuwatolea macho wawili hao, ni kutaka kuboresha sehemu ya kiungo ya kikosi chake, hasa ikizingatiwa mwishoni mwa msimu huu Mikel Arteta pamoja na Mathieu Flamini wataondoka kutokana na mikataba yao kufikia kikomo.

Wenger pia amethibitisha kupendezwa na huduma ya kiungo kutoka nchini Algeria na klabu ya Leicester City, Riyad Mahrez huku akisisitiza kuwa katika harakati za kuingia kwenye mipango ya kumsajili mwishoni mwa msimu huu.

Riyad Mahrez

Inaamiwa kwamba endapo Mahrez atasajiliwa na Arsenal, Wenger atamuachia Theo Walcott ambaye ameshindwa kudhihirisha ubora wa kupambana na kufikia lengo la kutwaa taji la nchini England kwa kusaidiana na wengine kikosini.

Mahrez ambaye mwanzoni mwa juma hili alitangazwa kuwa mchezaji bora wa chama cha wachezaji wa kulipwa nchini England (PFA), thamani yake ya usajili inakadiriwa kufikia Pauni million 25.

Miss Tanzania, Aliyekuwa Kamishna wa TRA, waanza kupeta mahakamani
Tyson Fury Atamba Kwa Umbile Lake