Watu wawili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro, wakituhumiwa kwa Mauaji ya Charles Maghashi (55),  aliyeuawa kwa kukatwa katwa na kitu chenye ncha kali.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polis Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama amesema tukio hilo limetokea Oktoba 29, 2023 Wilayani Malinyi na kumtaja mmoja wa watuhumiwa hao kuwa ni mke wa marehemu, Holo Jilia (45).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama.

Amesema, uchunguzi wa Polisi umebaini kuwa mke huyo wa marehemu alikula njama ya kumuua mumewe Maghashi, ambapo alimtuma Maela Athanas kutekeleza mauaji hayo.

Kamanda Mkama amebainisha kuwa, mauaji hayo yalipangwa kufanyika kwa ahadi ya malipo ya Shilingi 900,000 ambapo mke huyo wa marehemu alimtangulizia Maela Shilingi 50,000 kama malipo ya awali.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Novemba 3, 2023
Wachezaji Simba SC watengewa Milioni 500