Klabu ya Ashton United inayoshiriki Ligi daraja la Saba (7) Nchini England imetoa ofa ya mkopo wa siku 28 wa kumsajili mchezaji wa Manchester City, Erling Haaland kwa sababu mchezaji huyo hatashiriki Fainali za Kombe la Dunia.

Haaland hatakuwepo kwenye michuano hiyo nchini Qatar kwani Norway ilishindwa kufuzu na atakuwa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja.

Akizungumza kuhusu mpango huo meneja wa klabu hiyo Michael Clegg alisema “City haichezi, na tunataka kumsaidia kumweka sawa Erling na itakuwa na maana kubwa sana kuliko yeye kucheza gofu kwa wiki sita”

“Tunafikiri atakuwa anatufaa sana, na angeingia kwenye kikosi chetu vizuri sana.”

Ashton United wapo nafasi ya 11 wakiwa na alama 25 katika msimamo wa Ligi daraja la 7 wakifunga jumla ya mabao 23 na kuruhusu kufungwa mabao 21.

Erling Haaland aliyeifungu Manchester City mabao 18 katika michezo 13 aliocheza hadi sasa, alisajiliwa Etihad Stadium mwanzoni mwa msimu huu akitokea Borussia Dortmund, kwa ada ya Pauni Milioni 51.2.

Majaji wapitisha sheria mpya ya kuchapa, kukata mkono
Adel Zrane: Nipo tayari kurudi Simba SC