Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limemkamata mfanyabiashara Maila Majula (29), mkazi wa Makongo juu kwa kutoa taarifa za uongo katika kituo cha Polisi Msimbazi kuwa kaibiwa gari.

Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Jumanne Muliro amesema kwamba mfanyabiashara hayo ambaye ni Mkazi wa Makongo Juu, alitoa taarifa za uongo kuwa gari lake namba T.303 DPS aina ya Toyota IST rangi ya Bluu limeibiwa.

“Uchunguzi umebaini kuwa mtuhumiwa alipewa sh Milioni 10 na kaka yake ili akaziweke Benki matokeo yake akazitunia kwa matumizi yake binafsi na kuamua kutengeneza tukio la kufkikirika kuwa pesa ile na gari viliibwa wakati yeye aliposhuka kwa muda na aliporudi hakukuta gari iliyokuwa na pesa.” amesema Muliro na kuongeza

“Baada ya kumtilia mashaka mtoa taarifa ilibainika kuwa taarifa hizo ni za uongo, na ilibainika gari hilo amelificha maeneo ya Tabata kwa Swai ambako lilipatikana kabla ya kwenda kituoni kutoa taarfa za kuibiwa kwa Gari hilo.” amesema

Masau Bwire: Simba msije na matokeo mfukoni
Habari kubwa kwenye Magazeti leo, Februari 16, 2022