Mbunge wa Nanyamba, Abdallah Chikota (CCM) ameishauri serikali kutoa kibali maalum cha ajira ya watumishi wa sekta ya elimu na afya ili kupunguza upungufu mkubwa uliopo katika sekta hizo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Pia ameshauri Serikali kutekeleza azma ya kukipandisha Chuo cha Walimu Mtwara kuwa Chuo Kikuu Kishiriki cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kama ilivyo Chuo cha Walimu Dar es Salaam(DUCE) na kile cha Mkwawa (MUCE).

Chikota ametoa ushauri huo alipokuwa akichangia taarifa ya shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii katika kikao cha Bunge kilichofanyika bungeni Dodoma.

Hivyo, Chikota amesema mamlaka za Serikali za Mitaa zinaupungufu mkubwa wa idadi ya walimu na watumishi wa kada ya afya na kuiomba Serikali kuchukua hatua za makusudi kuhakikisha kwamba kibali maalumu kinatolewa kwa ajili ya ajira ya walimu na watumishi wa sekta ya afya.

Amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu imefanya kazi kubwa ya kujenga madarasa 15,000, mabweni 50 na vituo vya afya manufaa yake hayataonekana sana kama upungufu wa watumishi ukiendelea kuwepo.

Makundi ndani ya CCM ni haramu- Lusinde
TFF yatangaza Makundi Ligi ya Mikoa 2022