Klabu ya Simba SC imetambulisha Rasmi Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Augustine Okrah, kwa Mashabiki na Wanachama wa Klabu hiyo ya Msimbazi.

Simba SC imemtambulisha mchezaji huyo kupitia Simba APP na Kurasa zake za Mitandao ya Kijamii, leo Jumatano (Julai 13), saa saba mchana.

Okra amesajiliwa Simba SC akitokea Bechem United ya nchini kwao Ghana, kwa mkataba wa miaka miwili.

Inadaiwa Kiungo huyo amekamilisha usajili wake Msimbazi kwa dau la dola za Kimarekani 120,000 ambazo ni zaidi Shilingi Milioni 280 za Kitanzania.

Msimu uliopita Okrah mwenye umri wa miaka 28 alifunga mabao 18 (Ligi Kuu ya Ghana 14 na Kombe la FA 4), huku akitoa pasi saidizi (assist) 10 (Ligi Kuu 6 na Kombe la FA 4), akiwa na kikosi Cha Benchem United.

Kabla ya kutua ya kutua Simba SC, Okrah amewahi kuitumikia Asante Kotoko, RB Ghana FC na North East FC (zote za Ghana), Al Merreikh na Al Hilal (Sudan), Hacken (Senegal) na Smouha FC (Misri).

Serikali yatoa tamko ugonjwa mpya Lindi
Rais ateua mrithi wake, akimbia nchi