Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameielekeza Mamlaka ya Maji Arusha – AUWSA kushughulikia na kutatua kwa wakati kero za Wananchi.

Maelekezo hayo, yametolewa katika kikao kazi alichokifanya na Bodi ya Wakurugenzi pamoja na Menejimenti ya AUWSA hii leo Machi 1, 2023 Mkoani Arusha.

Amesema, “Watendaji wasizoe shida za wananchi, Kero na Matatizo yote kama vile Maunganisho mapya, mivujo, ankara, na huduma kwa wateja yasikilizwe na kushughulikiwe kwa wakati.”

Aidha, ameitaka AUWSA kuhakikisha wananchi wa Jiji la Arusha wanapata huduma ya Maji iliyoimarika na inayoridhisha na kwenye changamoto, AUWSA ishirikiane na viongozi wa jamii husika katika kupata suluhisho kwa manufaa ya Watanzania kwa Ujumla.

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi AUWSA, Balozi Mstaafu Daniel Ole Njoolay alimshukuru Waziri wa Maji kwa kutenga muda wake na kuongea na Bodi ya wakurugenzi na menejimenti ya AUWSA kwa lengo la kuboresha huduma inayotolewa na Mamlaka kwa Wananchi wa Jiji la Arusha.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa AUWSA Mhandisi Justine Rujomba, ameeleza kuwa Menejimenti na watumishi wote wa wamepokea maelekezo yote na ushauri uliotolewa katika kikao hicho, na kama ilivyoelekezwa na Waziri Kwamba AUWSA iendelee kujiimarisha kwenye maswala kama uadilifu, uaminifu, na mahusiano kwa wateja na hivyo ndivyo itakavyofanyika kwa manufaa ya wananchi wa Jiji la Arusha.

Shilogile atafuta muarobaini mauaji Kagera
Dkt. Ndunguru: Udanganyifu chanzo wadudu waharibifu wa mimea