Kikosi cha Azam FC kimewasili mkoani Kilimanjaro kikotokea jijini Tanga, baada ya kumaliza mchezo wake wa mzunguuko wa kwanza wa ligi Kuu Tanzania Bara 2021/22 dhidi ya Coastal Union.

Azam FC wamewasili mapema mkoani humo, kwa ajili ya kuweka kambi ya siku kadhaa kabla ya kupambana na Maafande wa jeshi la Polisi (Polisi Tanzania FC), mwishoni mwa juma hili katika mchezo wa mzunguuko wa pili wa Ligi Kuu.

Uongozi wa klabu hiyo yenye maskani yake jijini Dar es salaam, umetoa ufafanuzi wa kuamrisha kikosi chao kuelekea Kilimanjaro siku kadhaa kabla ya mchezo kwa kusema, itawasaidia wachezaji kuzoea hali ya hewa kabla ya kupambana na wenyeji wao Jumamosi (Oktoba 02), katika Uwanja wa Ushirika.

Kikosi cha Azam FC kinachonolewa na Kocha kutoka nchini Zambia George Lwandamina, kina kazi ya kusaka alama tatu, baada ya kuambulia alama moja kwenye mchezo uliopita dhidi ya Coastal Union uliomalizika kwa sare ya bao 1-1, juzi Jumatatu (Septamba 27) kwenye Uwanja wa CCM Mkwakwani.

Matola awatuliza mashabiki Simba SC
KMC FC wachimba mkwara ugenini