Klabu ya Azam FC imeweka wazi kuwa inahitaji kufanya vizuri kwenye michezo yao iliyobaki pamoja na kuongeza nguvu kwenye Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ linaloshikiliwa na Young Africans.

Azam FC imekata tiketi Robo Fainali ya hatua ya baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mapinduzi kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Timu hiyo ipo chini ya Kocha Mkuu, Kali Ongala ambaye ameweka wazi kuwa inahitaji kutwaa taji hilo ambalo mabingwa watetezi ni Young Africans.

Ongala amesema kuwa wachezaji wapo tayari na wanalitaka kombe hilo ambalo ni muhimu.

“Hili ni kombe muhimu kwetu na wachezaji wanalitaka hili kombe hivyo tutapambana kufikia malengo ambayo tunahitaji kufikia.” amesema Ongala.

Upande wa Ligi Kuu Azam FC ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi hiyo ikiwa na alama 47 baada ya kucheza michezo 24, ikitanguliwa na Simba SC yenye alama 54, huku Young Africans ikiwa kileleni kwa kufikisha alama 62.

Makala: Siri ya Mwanamke kujikomboa
Opah Clement kutambulishwa Beskitas