Kiungo kutoka Uganda Khalid Aucho anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Young Africans kitakachoikabili AS Real Bamako ya Mali, leo Jumatano (Machi 08).

Young Africans itakua mwenyeji wa mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam saa moja usiku, huku ikihitaji ushindi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutinga Hatua ya Robo Fainali.

Afisa Habari wa Young Africans Ally Kamwe amesema, Kiungo huyo yupo FIT baada ya kukabiliwa na majeraha ya michubuko ya Goti, aliyoyapata kwenye mchezo dhidi ya AS Real Bamako uliopigwa mjini Bamako-Mali mwishoni mwa mwezi Februari.

Kamwe amesema: “Khalid Aucho ambaye aliumia katika mchezo wa kwanza naye yupo fiti na atapatikana katika mchezo wetu hivyo hakuna namna nyingine ambayo watapona hwa Real Bamako, mashabiki wanatakiwa waje wakiwa wanajiamini kupata furaha.”

Hadi sasa Young Africans imekusanya alama 04 baada ya kucheza michezo mitatu ikiwa nafasi ya pili katika msimamo wa Kundi C, ikitanguliwa na AS Monastir ya Tunisia yenye alama 07.

TP Mazembe ya DR Congo ipo nafasi ya tatu kwa kuwa na alama 03, na AS Real Bamako inaburuza mkia wa Kundi C ikikusanya alama 02.

Opah Clement kutambulishwa Beskitas
Mayele aahidi furaha Uwanja wa Mkapa