Klabu ya soka ya Azam FC imezidi kupiga hatua za kimaendeleo baada ya kufungua rasmi duka lake la vifaa vya michezo.

Duka hilo limefunguliwa hivi karibuni katika mtaa wa Swahili na Mkunguni uliopo maeneo ya Kariakoo sokoni jijini Dar es salaam.

Duka hilo ni mahususi kwa ajili ya kuuza vifaa vya michezo vya klabu hiyo ambavyo si feki.

Kwa mujibu wa video fupi iliyowekwa kwenye ukurasa wa facebook wa klabu hiyo, duka hilo linauza jezi, bukta, kofia, soksi, fulana za kawaida pamoja na vifaa vingine vinavyohusu klabu hiyo.

Lengo la Azam FC kufanya hivyo ni kutengeneza mazingira mazuri ya kuuza jezi zao halali na kuziba mianya ya watu wengine kuvamia mapato ya jezi zao.

Azam FC imefanya uamuzi huo huku timu kongwe za Simba na Yanga zikiwa bado hazijaweka mipango sahihi ya kuhakikisha jezi zao haziuzwi kiholela.

Mara kadhaa klabu hizo zimekuwa zikielezea mipango yao kuhusu udhibiti wa jezi feki lakini utekelezaji wake bado umekuwa hafifu.

Anne Makinda Ajiweka Kando Ya Uspika Bunge Lijalo
Jamie Vardy Kumkalisha Benchi Wayne Rooney