Aliyekuwa Spika wa Bunge la Kumi, Anne Makinda ameamua kukaa kando ya mbio za Uspika wa Bunge la 11, siku chache baada ya kufanya kampeni kuwania nafasi hiyo kwa mara nyingine.

Taarifa za kuaminika zimeeleza kuwa Mama Makinda aliamua kuchukua uamuzi huo wa kujiweka kando ya mchuano huo baada ya kushauriwa na watu wake wa karibu kufuatia dalili walizoziona kwenye mchakato huo pamoja na mambo mengine.

Awali mama Makinda alidaiwa kuanza kampeni kupitia ujumbe mfupi alioutuma kwa wabunge wateule kupitia simu za mkononi akiwapongea na kuwaomba kumuunga mkono kuwa Spika wa Bunge la 11.

“Mimi ndugu yako kwa unyenyekevu na heshima kubwa kwa ko kama mbunge wangu, naomba kugombea uspika kwa mara nyingine, kwa msaada w Mwenyezi Mungu nakutegemea sana naomba uniunge mkono. Asante kwa ukarimu wako,” ilisomeka sehemu ya ujumbe unaoaminika kuwa ulitumwa na Anna Makinda kwa wabunge wateule.

Hata hivyo, hadi pazia la kuchukua na kurudisha fomu za kuwania Uspika wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linafungwa, Mama Anna Makinda alikuwa hajarudisha fomu yake hivyo kuonesha dhahiri kuwa ameachana na mpango huo.

Makada 21 wa CCM wamejitokeza kuwania nafasi ya Uspika wa Bunge.Dkt. Emmanuel Nchimbi, Samwel Sitta, Dkt Didas Masaburi, Balozi Philip Marmo, Mussa Hassan ‘Zungu’, Job Ndugai, Abdallah Mwinyi ni miongoni mwa majina ya makada wa CCM waliojitokeza kuwania nafasi hiyo.

CCM Yafunika Tena
Azam FC Yaendelea Kujiimarisha Kibiashara