Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea kuonesha kuwa bado kina mizizi mikubwa nchini na wananchi wengi bado wana imani nacho kuanzia ngazi za serikali za mitaa.

Hiyo imeendelea kubainika baad ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutoa mgawanyo wa idadi ya madiwani wa viti maalum ambao CCM imepata viti 1,021 huku wapinzani kwa ujumla wakipata viti 371 nchi nzima.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva ameeleza kuwa Tume hiyo imetoa mgawanyo wa viti maalum vya udiwani huku wakisubiri uchaguzi wa udiwani katika kata 34 ambazo hazikufanya uchaguzi ambazo zitatoa madiwani 14 wa viti maalum.

Kwa mujibu wa  NEC, Jumla ya idadi ya madiwani wa viti maalum nchi nzima ni 1,392.

Jaji Lubuva alitaja kwa kila chama na idadi ya madiwani waliopata kwenye mabano kuwa ni CCM (1,021), Chadema (280), CUF (79), ACT- Wazalendo (6) na NCCR Mageuzi (6).

“Kwa mujibu wa Sheria Nec imepewa mamlaka ya kushughulikia na kutangaza Viti Maalum vya Madiwani Wanawake visivyopungua 1/3 ya madiwani wa kuchaguliwa katika kila halmashauri ambayo 1/3 ya 3,975 ni viti 1,406,” alisema Jaji Lubuva.

Chama Cha Mapinduzi kiliibuka na ushindi mnono katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu baada ya kushinda katika nafasi ya urais, kuongoza katika majimbo mengi ya ubunge huku wakipata sehemu kubwa zaidi ya gawiwo la wabunge wa viti maalum ukilinganisha na vyama vya upinzani vilivyounda Ukawa.

Rio Ferdinand Asusia Mchezo Maalum, Kisa John Terry
Anne Makinda Ajiweka Kando Ya Uspika Bunge Lijalo