Aliyekua beki wa klabu za Leeds Utd, Man Utd pamoja na QPR, Rio Gavin Ferdinand, ametangaza kujiondoa kwenye kikosi cha Uingereza ambacho kitacheza mchezo wa hisani mwishoni mwa juma hili.

Ferdinand, ametangaza maamuzi hayo, kutokana na dhamira aliyojiwekea ya kutokukutana na beki na nahodha wa klabu ya Chelsea John Terry ambaye ni sehemu ya kikosi cha Uingereza ambacho kitacheza dhidi ya timu maalum ya dunia kwenye uwanja wa Old Trafford.

Ferdinand, ambaye alitangaza kustaafu soka May 30 mwaka huu, aliweka dhamira hiyo kutokana na kuchukizwa na maneno ya ubaguzi wa rangi aliyowahi kuyatoa John terry dhidi ya ndugu yake Anton Ferdnand miaka mitatu iliyopita wakati wa mchezo wa ligi ya nchini Engalnd.

Kutokana na tukio hilo John Tarry aliushtua ulimwengu na aliadhibiwa na chama soka nchini Engalnd FA, kwa kufungiwa michezo kadhaa sambamba na kuvuliwa unahodha wa timu ya taifa ya nchi hiyo, hali ambayo ilipelekea mchezaji huyo kujiuzulu kuwa sehemu ya timu iliyokwenda kucheza fainali za mataifa ya Ulaya mwaka 2012.

Katika mchezo huo wa hisani ambao umeandaliwa na UNICEF, kikosi cha Uingereza kinatarajiwa kuwa na mchezaji nguli duniani David Beckham na wengine ni Andy Cole, Fabio Cannavaro, Alessandro Nesta and Massimo Ambrosini.

Rooney: Namkubalia Sana Diego Costa
CCM Yafunika Tena