Nahodha na Mshambuliaji wa Man Utd, Wayne Rooney amekiri kupendezwa na uchezaji wa mshambuliaji wa klabu ya Chelsea Diego Da Silva Costa.

Rooney amekiri kuwa shabiki wa mshambuliaji huyo, kwa kutoa siri ya kumpigia kura wakati wa kinyang’amyiro cha tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa chama cha wachezaji wa kulipwa nchini England, PFA mwishoni mwa msimu uliopita.

Rooney, amesema anaamini Costa ni mchezaji mwenye sifa za kipekee na amekua akidhihirisha ubora wake anapokua uwanjani tena linapokuja suala la kuitafutia ushindi klabu yake ya Chelsea.

Amesema mara kadhaa amekua akimfuatilia mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, na amebaini kuna mambo mengi ambayo yamekua yakimsaidia kufikia malengo yake ya kupachika mabao.

Hata hivyo, huenda kauli hiyo ya Wayen Rooney ikawashangaza mashabiki wa soka walio wengi, kutokana na kumtazama Costa kama mchezaji mtukutu ambaye mara nyingi amekua akionyesha utovu wa nidhamu dhidi ya wachezaji wa timu pinzani.

Rooney, alilazimika kumzungumzi Costa, kufuatia mchezo wa hii leo, ambapo kikosi cha England kitapambana na Hispania na anatarajiwa kuwa na mshambuliaji huyo ambaye alisajiliwa na Chelsea akitokea Atletico Madrid mwaka 2014.

Msimu uliopita Costa, alifanikiwa kufunga mabao 20, ambayo yalichochea kasi ya klabu ya Chelsea kutwaa ubingwa wa nchini Engalnd.

Azam FC Kuanzisha Mradi Kuinua Soka La Vijana
Rio Ferdinand Asusia Mchezo Maalum, Kisa John Terry