Meneja wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho amesema Faini ya Pauni 50,000 aliyotozwa na chama cha soka cha England (FA) ni fedheha.

Mourinho amepewa Adhabu hiyo ya faini pamoja na Kifungo cha mchezo mmoja, ambacho kimesimamishwa kwa kuchunguza mwenendo wake baada ya kupatikana na hatia ya utovu wa nidhamu kufuatia kauli yake kuhusu Refa Robert Madley mara baada ya kufungwa 3-1 na Southampton.

Mourinho ameeleza pauni 50,000 ni fedheha, uwezekano wa kufungiwa Mechi 1 ni kitu cha kushangaza!”

Mourinho pia alimchimba Meneja wa Arsenal Arsene Wenger bila kumtaja jina alipogusia kuwa Wenger, alisema nini mara baada ya kuchapwa 2-0 na Chelsea Mwezi uliopita.Wenger alidai Refa wa Mchezo ule Mike Dean, alikuwa ‘dhaifu’ na ‘asiefahamu’.

Mbali ya hilo, Wenger pia hakuadhibiwa na FA Oktoba 2014 wakati alipomsukuma Mourinho, aliyekuwa eneo lake la ufundi, Chelsea ilipopambana na Arsenal.

Utafiti Wabaini Tabia Hizi Kwa Watu Wenye ‘Tattoo’ Mwilini
Chadema Wadai Wamebaini Wachina, Wazungu Kwenye orodha Ya Wapiga Kura