Msanii Baraka The Prince amekanusha kuzaa mtoto na video queen Careen ambaye ni mkazi wa Arusha, kama ambavyo imesambaa mitandaoni.

Baraka amekanusha tuhuma hizo pindi alipofanyiwa mahojianao na kusema kwamba hajazaa na binti huyo na wala hajawahi kukutana naye kimwili.

Licha ya kuchezwa sauti ya binti huyo ikiongolea kuwa Baraka ndiye baba wa mtoto huyo Baraka amesema ingawa mama mtoto kasema ni wake lakini sio kauli ya kuaminika kwani ameshapatitia mikasa mbalimbali kama hiyo.

“Nina mtoto mmoja yuko Arusha, mama anaitwa Farida, ni mtoto wangu, hizo stori zingine sio kweli”, amesema Baraka The Prince.

Pamoja na hayo Baraka amekanusha taarifa za kuachana na mpenzi wake, na kusema kwamba bado wapo pamoja.

 

Manara: Ni aibu ya mwaka
Video: Lissu aanika kila kitu risasi iliyobaki mwilini mwake, Marufuku kufyatua fataki Dar