Msanii chipukuzi anayefanya vizuri katika muziki wa bongo Fleva, Nandy ameachia nyimbo yake mpya inayofanya vizuri upande wa audio na video.

Nandy ambaye ni msanii mchanga aliyepata umarufu kupitia wimbo wake wa nagusagusa ambao ulimfanya kwa mara ya kwanza kushiriki katika tamasha kubwa Tanzania la Fiesta kutokana na ubora wa nyimbo huo.

Pia siku chache zilizopita msanii Nandy katika tamasha la Fiesta mwaka huu ameingia katika mtafaruku mkubwa na msanii mkongwe Ray C, baada ya Nandy kuimba nyimbo za Ray C, na kumfanya Ray C amfungukie na kumtupia madongo akidai wangeona umuhimu wake wangemuita katika tamasha hilo la Fiesta hivyo hapendezewi na tabia ya msanii hiyo kuimba nyimbo zake ilihali yeye yu hai.

Video ya Kivuruge kwa sasa upande wa You Tube inafanya vizuri na kushika nafasi ya pili kuangaliwa na watu wengi katika mtandao huo.

Kuangalia video hiyo bonyeza link hapo chini.

LIVE: Rais Magufuli akiweka jiwe la msingi jengo la ofisi ya Takwimu
Wasira: Katiba mpya imenibeba