Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano na msemaji wa Klabu ya Simba SC, Haji Manara amekerwa na kusikitishwa kwa kitendo cha klabu yake ya Simba jana kufungwa kwa njia ya penati na kuondolewa kwenye michuano ya Azam Sports Federation Cup.

Haji Manara kupitia kurasa wake wa twitter amenung’unika vikali kwa klabu yake ambayo ni mabingwa watetezi wa Azam Sports Federation Cup, Simba kupigwa na Green Warriors na kuondolewa katika michuano hiyo kwa penati 4-3.

“Shame!! Aibu!!!Fedheha!!! Haivumiliki!!!Tumewakera fans wetu zaidi ya twenty millions… nimeumia kuliko siku zote toka nimeanza kazi Simba..Aibu ya mwaka” aliandika Haji Manara

Majaliwa awanusuru Viongozi 19 kutiwa mbaroni
Baraka The Prince amkana mwanae