Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe amemtaka kocha mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM na Makocha wasaidizi kuwa na umoja na ushirikiano ili kufikia malengo ya Chama na Serikali
Ametumia ukurasa wake wa Twitter kuwasilisha ombi lake hilo kwa uongozi wa juu uliochaguliwa katika mkutano mkuu wa tisa wa CCM mjini Dodoma.
“Kocha na makocha wasaidizi tunaamini, tumewaamini, tuliwaamini Kila la kheri katika kukiongoza Chama Chetu 2017-22. tuunganishe nguvu ili tuweze kufikia mafanikio kwa pamoja,”ameandika Bashe
Aidha, Bashe amehimiza kufanya mambo kwa umoja ili kupiga hatua kubwa tofauti na mtu akifanya vitu peke yake atapiga hatua kidogo, Uongozi huo mpya utahudumu kwa muda wa miaka mitano 2017 hadi 2022.
-
Heche: Serikali haijawahi kupambana na rushwa
-
Ikosoeni serikali kwa utaratibu- JPM
-
Makamba awamwagia sifa waasisi wa Taifa
Hata hivyo, Rais Magufuli alichaguliwa kwa kura zote 1821 za wajumbe wa mkutano mkuu, huku Rais Ali Mohamed Shein wa Zanzibar pia akichguliwa katika nafasi ya Mwenyekiti Zanzibar wakati nafasi ya Makamu Mwenyekiti alichaguliwa, Philip Mangula.