Hali ya sintofahamu imewakumba wadau wa muziki wa Bongo Flava nchini baada ya Ben Pol kumpa makavu Ali Kiba kwenye mtandao wa Twitter.

Ben Pol ameandika ujumbe kwa Ali Kiba na kumueleza kwa neno la lugha ya kigeni kuwa anahisi watu wanamjaza sifa nyingi au kumuweka kwenye viwango vya juu wakati hana uwezo wanaoudhani, yaani ‘Overrated’. Kitu ambacho Ben anaamini kinamgharimu Ali.

“Bro @officialalikiba mimi naona kama unakuwa Overrated halafu inakugharimu… Au haikugharimu?” ametweet Ben Pol.

Haijafahamika chanzo cha Ben Pol kutweet dongo hilo kwa Ali ambaye ameshiriki naye Coke Studio jijini Nairobi.

Naye Ali Kiba hakusita kujibu tweet ya Ben Pol kwa mtindo unaoonesha kitu.

“INSHAALLAH Heri @iambenpol asante kwa kunyoosha kidole. Sio makosa yako ni dua inafanya kazi yake #KingKiba” alijibu Ali Kiba.

Kunani kati wakali hawa wa ‘Cheketua’ na ‘Sophia’?

Sasa Ni Rasmi, Chelsea Yamfungashia Virago Mourinho
Hans Poppe Arejesha Kombora Kwa Justice Majabvi