Fununu za mshambulaiji kutoka nchini Ufaransa Karim Mostafa Benzema za kuondoka Real Madrid katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi zimeingia dosari, baada ya taratibu zilizoanza kuchukuliwa na viongozi wa klabu hiyo za kumsainisha mkataba mpya.

Taarifa zilizoripotiwa na JDD zimeseama kuwa, Benzema atasaini mkataba wa miaka minne wa kuendelea kuitumikia Real Madrid hadi mwaka 2021.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa jiaka 34, alikua anatajwa huenda akaondoka klabuni hapo, endapo meneja Zinedine Zidane atakubali kumsajili Kylian Sanmi Mbappé Lottin wa mabingwa wa Ufaransa AS Monaco.

Kwa mara ya mwisho Benzema alisaini mkataba wa miaka minne mwaka 2014 ambao unatarajia kufikia kikomo mwaka 2018.

Endapo Benzema atasaini mkataba mpya kama inavyoelezwa atakua na faida ya ongezeko la mshahara la Euro milioni 8 kwa kila mwaka.

Benzema alijiunga Real Madrid mwaka 2009 akitokea kwa mabingwa wa Ufaransa wakati huo Ulympic Lyon.

Samir Nasri Atuma Salamu Etihad Stadium
Young Africans Kuwasili Mchana Kweupeee