Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania bara Young Africans kinatarajia kuwasili jijini Dar es salaam leo mchana kikitokea kisiwani Pemba kilipoweka kambi ya kujiandaa na mchezo wa Ngao Ya Jamii utakaochezwa kesho kwenye uwanja wa Taifa.

Young Africans, watapambana na mahasimu wao Wekundu Wa Msimbazi Simba katika mchezo huo, ambao umepangwa kuanza mishale ya saa kumi na moja jioni.

Tayari kikosi cha Simba kimeshawasili jijini Dar es salaam tangu jana, kikitokea kisiwani Unguja, kilipokua kimeweka kambi ya majuma mawili kujiandaa na mchezo huo.

Afisa Habari wa Young Africans Dismas Ten amesema kikosi chao kitawasili kwa usafiri wa ndege, na kisha kitaenda kambini kusubiri mchezo huo.

Dismas amesema wachezaji watatu wataukosa mchezo huo, kutokana na majeraha yanayowakabili. Wachezaji hao ni Obrey Chirwa, Geofrey Mwashiuya na Beno Kakolanya.

Benzema Kubaki Real Madrid Hadi 2021
India yafuta sheria ya kuwapa talaka wanawake kirahisi kwa ‘WhatsApp’