Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye ametoa wito kwa Wakenya kuilinda demokrasia yao ili kuepuka kutumbukia kwenye lindi la maovu kama yanayotokea nchini Uganda

Wito wa Besigye, umetolewa wakati wa kongamano la masuala ya haki za binadamu lililofanyika Nairobi likiwa na ajenda ya kuadhimisha miaka miwili tangu wahanga wa ukatili walipoteswa na maafisa wa usalama wa Uganda kabla ya uchaguzi mkuu.

Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye. Picha ya AP

Besigye ambaye ni mzoefu wa kisiasa, pia amesema kuhusu kauli za hivi karibuni za Mbunge wa Fafi Yakub Salah kuwa na majaribio ya kuondoa kipengele cha muda wa rais kuhudumu, zinatia shaka kwani ni ishara mbaya na kuwataka Wakenya kuwa imara.

Wahanga hao wa ukatili wa Uganda, walisimulia maovu yaliyowasibu kabla ya uchaguzi mkuu mwaka 2020 na kuelezea jinsi walivyoteswa, kupigwa, kukamatwa kwa nguvu na maafisa wa usalama ikiwa imesalia miezi miwili kabla ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.

Watoto walia na Serikali ndoa za utotoni
Aliyetawala tangu 1979 awania muhula wa sita wa Urais