Rais mteule wa Marekani Joe Biden ameteua maafisa wa ngazi ya juu kusimamia uchumi wa Marekani unaoathiriwa na janga la virusi vya Corona.
Miongoni mwa walioteuliwa ni aliyekuwa mwenyekiti wa Benki Kuu ya Marekani Janet Yellen, ambaye anakuwa mwanake wa kwanza kuwa waziri wa fedha katika historia ya miaka 231 ya wizara hiyo.
Biden amemteua Neera Tanden, kuwa mkuu wa ofisi ya kusimamia utawala na bajeti ya serikali, iwapo ataidhinishwa na senate, Tanden atakuwa mwanamke wa kwanza, Mmarekani mwenye asili ya Afrika kuongoza idara hiyo.
Wally Adeyemo, ameteuliwa kuwa naibu wa waziri wa fedha, akiwa mmarekani wa kwanza mwenye asili ya Afrika kuteuuliwa katika nafasi hiyo wengine walioteuliwa ni Pamoja na mchumi Cecilia Rouse, kuwa mkuu wa baraza la washauri wa uchumi white house ya Marekani.
Janga la Corona limeathiri sana uchumi wa Marekani ambao ndio mkubwa zaidi duniani.
Itakumbukwa Novemba 31, mwaka huu Biden aliteua wanawake kuongoza timu nzima ya mawasiliano white house.